Job 40

1 a Bwana akamwambia Ayubu:
2 b“Je, mwenye kushindana na Mwenyezi aweza kumsahihisha?
Mwenye kumlaumu Mungu na ajibu.”

3Ndipo Ayubu akamjibu Bwana:
4 c“Mimi sistahili kabisa: ninawezaje kukujibu wewe?
Nauweka mkono wangu juu ya kinywa changu.

5 dNimesema mara moja, lakini sina jibu;
naam, nimesema mara mbili,
lakini sitasema tena.”

6 eNdipo Bwana akasema na Ayubu kutoka upepo wa kisulisuli:
7 f“Jikaze kama mwanaume;
nitakuuliza maswali, nawe yakupasa unijibu.


8 g“Je, utabatilisha hukumu yangu?
Utanilaumu mimi ili kujihesabia haki mwenyewe?

9 hJe, una mkono kama wa Mungu,
nawe waweza kutoa sauti ya ngurumo kama yake?

10 iBasi jivike mwenyewe utukufu na fahari,
nawe uvae heshima na enzi.

11 jFungulia ukali wa ghadhabu yako,
mtafute kila mwenye kiburi umshushe,

12 kmwangalie kila mtu mwenye kiburi na umnyenyekeze,
waponde waovu mahali wasimamapo.

13 lWazike wote mavumbini pamoja;
wafunge nyuso zao kaburini.

14 mNdipo mimi mwenyewe nitakukubalia
kuwa mkono wako mwenyewe wa kuume unaweza kukuokoa.


15 n“Mwangalie mnyama aitwaye Behemothi,
Huyu alikuwa mnyama wa nyakati za zamani ambaye hajulikani hasa ni gani.

niliyemuumba kama nilivyokuumba wewe,
anayekula majani kama ng’ombe.

16 pTazama basi nguvu alizo nazo kwenye viuno vyake,
uwezo alio nao kwenye misuli ya tumbo lake!

17 qMkia wake hutikisika kama mwerezi;
mishipa ya mapaja yake imesukwa pamoja.

18 rMifupa yake ni bomba za shaba,
maungo yake ni kama fito za chuma.

19 sYeye ni wa kwanza miongoni mwa kazi za Mungu,
lakini Muumba wake anaweza kumsogelea kwa upanga wake.

20 tVilima humletea yeye mazao yake,
nao wanyama wote wa porini hucheza karibu naye.

21 uHulala chini ya mimea ya yungiyungi,
katika maficho ya matete kwenye matope.

22 vHiyo mimea ya yungiyungi humficha kwenye vivuli vyake;
miti mirefu karibu na kijito humzunguka.

23 Wakati mto ufurikapo, yeye hapati mshtuko wa hofu;
yeye yu salama, hata kama Yordani ingefurika hadi kwenye kinywa chake.

24 wJe, mtu yeyote anaweza kumkamata yeye akiwa macho,
au kumnasa kwa mtego na kutoboa pua yake?

Copyright information for SwhKC